KIFO CHA KANUMBA CHALIZA WENGI:MATUKIO KATIKA PICHA

 
Taarifa nilizozipata sasa hivi kutoka kwa mwigizaji Dino, ni kwamba kweli mwigizaji STEVEN KANUMBA amefariki dunia na inaaminika chanzo cha kifo chake ni baada ya kuanguka na kuanza kutoa mapovu hapohapo nyumbani kwake, alikua akiishi na mdogo wake anaitwa Fetty aliekua chumba kingine ambae amethibitisha kweli kwamba alimkuta kaka yake akiwa ameanguka.

HISTORIA FUPI YA MAREHEMU STEVEN KANUMBA

HISTORIA YAKE:
Steven Charles Kanumbaa alizaliwa Januari 8, mwaka 1984 mkoani Shinyanga kabla ya umauti kumfiia Aprili 6, mwaka 2012.
Elimu ya msingi alipata katika shule ya Bugoyi, na baadaye akajiunga na  sekondari ya Mwadui, kabla ya kuhamia Dar Christian Seminary.
Baada ya kumaliza Kidato cha Nne Dar Christian, Kanumba alijiunga na sekondari ya Jitegemee, Dar es Salaam pia kwa elimu ya Kidato cha Tano na Sita.
Ni ni wakati huo akiwa Jitegemee Kanumba alianza shughuli za sanaa katika Kundi la Kaole Sanaa Group la Magomeni, Dar es Salaam.
Baada ya kukomaa Kaole, Kanumba aliamua kuanzisha kampuni yake mwenyewe ya filamu na hadi anakutwa na umauti alikuwa mwigizaji anayefahamika Afrika nzima.
Ameshirikiana na wasanii wakubwa duniani kama Ramsey Nouah wa Nigeria na amefanya kazi na mastaa wengine kadhaa wa Nigeria.
Miongoni mwa filamu ambazo alifanya ni Dar To Lagos, She is My Sister, Ancle JJ, Oprah, Tufani, Johari, Gharika, Baragumu, Sikitiko Langu, Dangerous Desire, Cross My Sin, Village Pastor, Family Tears na kadhalika.
Hivi karibuni, alikaririwa akisema atagombea Ubunge katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015.
Kanumba atakumbukwa na wengi sana kwa ucheshi wake- upole na ushirikiano mzuri na wenzake katika kazi.
Kifo cha Kanumba ni pigo katika tasniya ya filamu Tanzania. Taifa limempoteza mtu ambaye alikwishaanza kuitangaza vema nchi kupitia sanaa hiyo na ambaye angetarajiwa kuitangaza zaidi katika anga za kimataifa zaidi kupitia sanaa hii.
Nigeria sasa wanajua Tanzania sasa filamu. Nchi nyingi za Afrika zinajua sasa nah ii sehemu ya kazi nzuri kwa Kanumba.
Mwenyewe aliwahi kukaririwa alifika hadi Hollywood hadi Marekani, ambayo ni ‘makka’ ya wacheza filamu. Kwa sasa mwili wa marehemu upo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam.
Mungu aiweke pema peponi roho ya marehemu. Amin.

Tumsaidie Mtoto Farid Rashid

Mtoto  Farid Rashid mwenye umri wa mwaka 1 na miezi 8 anasumbuliwa na tatizo la kuziba kwa mirija  inayosafirisha haja ndogo( mkojo) kati ya Figo na Kibofu cha mkojo. Baba Mzazi (Rashid Said)  wa mtoto huyo anawaomba msaada wadau mbalimbali ili aweze kumpeleka mtoto Farid nchini India kwa matibabu zaidi.

“Mwanangu anajisaidia kwa maumivu makali, sema kweli ni mateso makubwa kwa mtoto, naomba mnisaidie mwanangu apate matibabu” hayo ni maneno ya baba mzazi wa Farid (Rashid Said).

Akizungumza na Msimamizi wa Mtandao wa habari wa  MO BLOG Bi. Johari Kachwamba Ndugu Rashid Said amesema amemzungusha kwa matibabu mtoto Farid katika hospital mbalimbali za hapa nchini bila mafanikio ikiwa ni pamoja na kulazwa zaidi ya miezi mitatu(3) katika hospitali ya taifa ya Muhibili.

Katika juhudi za wazazi wa Farid kutafuta misada, wamefanikiwa kupata tiketi moja (1) ya ndege, dola 1,500 pamoja na Shilingi Milioni moja (1) lakini bado haitoshi.
Hata hivyo tayari wamefanikiwa kupata hati za kusafiria (Passport) na VISA ya nchini India ambayo inakoma (expire) 19-06-2012.

 Hivyo anaomba msaada wa kupata tiketi nyingine pamoja na gharama za matibabu.


Nambari ya simu ya baba mzazi ni 0655-000556 au wasiliana na MO BLOG kupitia nambari 0714-940992.

MAJINA YA WANAFUNZI WALIO CHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO 2012

JOKATE NA DIAMOND WAZUA BALAA JINGINE

ACHANA na kitendo cha Naseeb Abdul ‘Diamond’ kukataa kupokea fedha alizotuzwa na  zilipendwa wake, Wema Isaac Sepetu katika shoo ya Diamond are Forever ndani ya Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar Ijumaa iliyopita, kuna vitu vingine viliwaacha wadau na maswali kibao katika shoo hiyo

Wadau waliofurika ukumbi humo walikuwa wakifuatilia vitendo walivyokuwa wakifanya Diamond na  mlimbwende namba mbili wa Tanzania mwaka 2006, Jokate Mwegelo  hatua kwa hatua.