Sylvia Shally ajifungua



MNYANGE wa Ilala 2009/10, Sylvia Shally (pichani) amejifungua mtoto wa kiume Jumapili katika Hospitali ya Kairuki Mikocheni jijini Dar.

Kwa mujibu wa mnyange huyo ambaye alizungumza na gazeti hili akiwa nyumbani kwake Kinondoni jijini Dar es Salaam amejifungua salama kwa njia ya kawaida na kukikwepa kisu.
“Nimefurahi kupata mtoto wangu wa kwanza,” alisema Sylvia ambaye aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na marehemu Steven Charles Kanumba.
Hata hivyo, Sylvia amegoma kumtaja baba mzazi wa kichanga hicho.