(hii picha ni kutoka kwa Alpha Rwirangira )
Rais
Paul Kagame wa Rwanda amekua miongoni mwa marais wachache wa Ulimwengu
wanaopewa sifa nyingi za kweli kuhusu msimamo wao, mipango yao na hata
utekelezaji wa hiyo mipango waliyonayo.Kwa taarifa nilizonazo
Rais Kagame ameweza kuibadili Rwanda kwa kiwango kizuri sana ikiwa ni
pamoja na nchi kuwa safi, kukua kiuchumi, kujengeka kimpangilio pamoja
na ishu nyingine, sasa hivi sehemu kubwa ya mji wa Kigali umejengwa kwa
mujibu wa ramani inayotakiwa, nyumba za kuishi zilizo kwenye mpango
kama miji mingine ya nchi zilizoendelea, pamoja na barabara za ndani za
Kigali kuwekwa mawe kitaalamu kuondoa vumbi kwenye mji.
Nyumba zilivyojengwa kimpangilio kwenye mji wa Kigali.
Huu ni mfano wa jinsi Kigali Rwanda ilivyopangwa kujengwa katika miaka michache ijayo according to topboxdesign.
Hii
ndio Account ya Rais Paul Kagame kwenye twitter, Paul Kagame (54) ni
rais wa sita wa nchi hiyo ambayo ameiongoza kwa zaidi ya miaka kumi na
wengi wanaamini kama angeendelea kukaa madarakani kwa muda mrefu zaidi,
angeweza kuibadilisha Rwanda kwa kiwango kikubwa sana.