Voula Papachristou
.
Wakati
mashindano ya Olympic yakiwa yanaanza ijumaa, Mwanariadha wa Ugiriki
Voula Papachristou amefukuzwa na kuondolewa kushiriki mashindano hayo
baada ya kuandika maneno ya kibaguzi dhidi ya watu weusi kupitia page
yake ya mtandao wa kijamii wa twitter.
Aliandika “waafrika walivyojaa huku Ugiriki, afadhali hawa mbu wale, watapata chakula cha nyumbani kutoka magharibi mwa mto Nile”.
Japo
baadae aliomba msamaha kupitia hapo hapo Twitter, haikusaidia kutokana
na uzito wa kosa lenyewe ambalo halikuhitaji hata mzaha kulifanya.