baadhi ya magazeti ya jana
Juzi
Chama Cha CUF Kilifanya mkutano mkubwa wa hadhara katika viwanja vya
Jangwani.nilikuwepo binafsi nikichukua picha na kusikiliza hotuba
mbalimbali.pamoja na mambo mengine,CUF Inaonekana kutokuwasema vizuri
wana habari.na nilisikia mwenyewe kutoka hotuba za viongozi,isipokuwa
Lipumba pekee mashambulizi,ama vijembe kwa wanahabari.
Sasa
ni kweli upo mgogoro kati ya waandishi na CUF?,kama ndiyo,umesababishwa
na nini,na kama hakuna ugomvi,nini kinapelekea habari za CUF kutopata
uzito unaostahili kwenye vyombo vya habari? je yawezekana ni mikakati ya
washindani wao kisiasa yaani CCM na CHADEMA kwamba CUF wasipewe uzito?
na ama ni udhaifu wa idara ya habari ya chama cha CUF yenyewe kutotenda
kazi ipasavyo? maana nikiri pia kuwa japo mimi ni mwanahabari sikumjua
afisa habari wa CUF hadi juzi alipotambulishwa mkutanoni. Na katika
mengi ama yawezekana hii ni kutokana na CUF kushuka umaarufu kisiasa
kiasi kwamba habari zake hazivuti wasomaji? naomba mitazamo yenu.
Msaidizi wa Mwenyekiti,Dar