"WASANII WA KENYA WANALITAMANI SANA SOKO LA TANZANIA"....NCHAKALIH

Kuna mjadala mtamu sana wa wadau wa muziki wa Tanzania umefanyika Facebook kwenye wall ya aliyekuwa mtangazaji wa Clouds FM Reuben Ndege aka Nchakalih.
“Kila deejay na msanii wa kenya ambae nimekutana nae ndani ya wiki moja ya kuwa huku 254, analiangalia soko la TZ na kupanga kuja kufanya kweli.....ni changamoto kwetu kufanya kweli na kuhakisha tunawapa watz kile wanacho stahili ili kukabiliana na ushindani unaotarajiwa kuvuka mipaka ya EA, ” ameandika Nchakalih.

Baada ya status hiyo wadau wengine waliamua kusema yao pia na kuzungumzia kasoro za wasanii wa Tanzania zinazopelekea kushindwa kutoka nje ya mipaka.
Jimmy Blanks alisema, “There is discipline and structure in the composition of music and in it’s study, perfecting, and performance. NEGLECTING structure on the composition side generally produces an undesirable product. 
A lot of people won't like what i have to say BUT bongo artists lack foresight and business acumen in their work.”

“Tumewahi kulijadili hili mimi na wewe....na ulinipa experiences zako kama promoter pande za uingereza na baadhi ya wasanii wakubwa wa hapa bongo.....kama wataendelea kujilemaza na kutoangazia upande wa biashara....wataumia vibaya,”aliongeza Nchakalih.

Mie nashangaa sana wasanii wa bongo 24/7 ni kula bata tu. Wenzetu 24/7 wanatafuta soko la biashara. They are already conquering Southern Sudan. Kwa Kumbukumbu zangu I only know of A.Y. ndo kaenda kuperform huko. Tz music market is HUGE. I mean seriously ........ one year uzunguke mikoani and self promote na you are guaranteed to make money (Jimmy Blanks)

Josthers Peter aliandika, “Muziki ni biashara tena inayohitaj plan kubwa maana bidhaa yako itauzwa nch na mikoa mbalimbal sio duka et utawauzia wa2 wa karibu tu, wasanii wetu weng wametokea uswaz hawan elimu na biashara kubwa kama hii, je watu wanaowazunguka kwenye kaz yao wanawasimamia kwel kibiashara? mf mamenager wanasimamia biashara ya msanii we2 aliyetokea pale bugurun kwa mnyaman kweli au wao kazi yao n kutoa pesa ya kurekodi tu, hata hao akina 50 cent bila ya kusimamiwa na watu wenye upeo wa biashara wasingekuwa hapo walipo.”