"YMCMB NDO CHANZO CHA WATOTO WA KIUME KUVAA SURUALI KAMA CONDOM NA KUVAA MAVAZI YA KIKE".....NIKKI MBISHI

Si ajabu ulishakutana na vijana mjini waliovaa nguo na suruali zinazobana na ambazo zinakaribia kuanguka viunoni kwasababu ya mtepesho wa hatari kama Lil Wayne! Ama ulishakutana na msichana wa miaka 16 akiwa ametengeneza kope zake kwa kuzipaka rangi za ajabu ajabu ili afananane na Nicki Minaj!
Kitu cha kawaida zaidi kukutana na vijana waliovaa t-shirt zilizoandikwa YMCMB (Young Money Cash Money Billionares).
Sio kila mtu anafurahia mavazi ya wasanii hao wa Marekani. Infact, rapper Nikki Mbishi aka Baba Malcom, anawalaumu wasanii wa YMCMB kwa kuharibu vijana wa Tanzania.

“Hawa wadwanzi YMCMB ndo wamesababisha watoto wa kiume kuvaa mavazi ya kike na visuruali kama condoms,mbaya zaidi rangi zao ni njano,kijani,nyekundu,pink,purple,orange mpaka aibu mitaani,ukija kwenye hair cutz ndo mama yangu,mara rangi ya njano,pink n.k yaani ni MASHOGA TASLIMU!!!,” alisema Nikki kupitia Facebook.