
Kwa kujiamini kabisa, tunasema haijawahi katika historia ya Fiesta na
 show za muziki wa Tanzania msanii kusifiwa kwa kazi nzuri aliyoifanya 
kwenye stage kama ilivyokuwa kwa Mwana FA!
 Huenda sababu ikawa ni kukua 
kwa mitandao ya jamii kama Twitter ambapo mashabiki wana nafasi rahisi 
kutoa pongezi zao kwa msanii husika lakini seriously Mwana FA aka Binamu
 aliangusha performance kali pengine kuliko zote alizowahi kuzifanya 
kiasi cha jana kwenye Twitter kugeuka mjadala na hata kuifunika show ya 
Rick Ross ambayo nayo ilikuwa kali sana.
Mwana FA aliingia stejini kwa plan nzuri ya namna ya kuimba nyimbo 
zake. Tunahisi alifanya rehearsal na maandalizi ya maana. 
Akiwa na 
T-shirt nyekundu yenye maandishi ‘CAN’T STOP THE HUSTLE & GRIND na 
miwani iliyokuwa na mishikio yenye rangi nyekundu pia, alionekana smart 
kinoma.

FA alikuwa ameandaa nyimbo zaidi ya sita zilizohit kinoma na kuchagua
 kuziimba verse moja moja huku kila moja ikishangiliwa na mashabiki. Kwa
 kujiamini, FA aliyekuwa mcheshi muda wote aliweza kuongea na mashabiki 
kuliko msanii yoyote aliyepanda siku hiyo isipokuwa Rozay tu. 
‘Zipo nyingi, sasa ntafanyeje?’ alisikika FA mara nyingi baada ya 
kuwa anakatisha nyimbo zake ili kuimba nyingine.
 Unanitega, Mabinti, 
Binamu, Yalaiti, Habari Ndio Hiyo, Unajinua Unasikia, Naongea na wewe na
 zingine ziliamsha shangwe za wengi kwenye viwanja vya Leaders. 
Akiongea leo kwenye kipindi cha Power Breakfast kutoa shukrani kwa 
wananchi kwa jinsi walivyoiunga mkono Fiesta, mkurugenzi mtendaji wa 
Clouds Media Group, Joseph Kussaga, amesema wapo wamarekani waliomfuata 
na kumuuliza ‘who is that guy’ wakati FA alipokuwa kwenye stage.
Kwa namna yoyote ile, performance hiyo ya aina yake ya rapper huyo 
ambaye jina lake halisi ni Hamis Mwinjuma, imefungua ukurasa mwingine 
mpya wa heshima aliyonayo ndani na nje ya nchi na huenda ikampa michongo
 mingi zaidi. Kiukweli FA, amelitumia vema jukwaa la Fiesta na huo ndio 
tunauita ‘ukomavu’.
Hizi ni baadhi ya tweets zilizokuwa zikisifia show ya Mwana FA.

 
 
 
 
 
 
