Diamond na Raqey wakichagua picha ya kutumia kwenye cover ya wimbo wake mpya
Baada ya miezi kadhaa ya ukimya bila track mpya hewani hatimaye staa
wa ‘Mawazo’ Diamond Platnumz kesho anatarajia kuachia wimbo wake mpya.Ngoma hiyo ameipa jina la ‘Nataka Kulewa’ ambayo imefanywa na producer wa AM Records, Manecky.
Kupitia website yake, Diamond ameshare kwa mashabiki wake picha za utengenezaji wa cover ya ngoma hiyo uliosiomiwa na Raqey Mohamed wa I-View Media kampuni ambayo inamsimamia.
Kuhusu mipango ya video aliyoifanyia usaili wa models wiki kadhaa zilizopita Raqey amesema bado wanashughulikia permit na hivi karibuni alikuwa Dubai kwaajili ya kuweka mambo sawa.
Hizi ni baadhi ya picha hizo.