WAKATI hali ya kimaisha ikiwa tete kwa msanii anayefunika kwa urembo bongo movie Jackline Wolper, ambaye alikuwa akitembelea magari ya kifahari kila kukicha, sasa anachoambulia ni pole kwani shosti yake wa karibu Sintah, amedai kuwa kuachana kwao na ‘Dallas’ kutamfanya Wolper ayakumbuke magari yake ya zamani kama vile Noah.Wolper
ni msanii wa kwanza bongo kutembelea magari ya
kifahari tena baada ya kumpata jamaa huyo lakini awali kabisa alikuwa
akitembelea Noah, na inadaiwa kuwa sasa atakuwa akiyaona kwa macho watu wakiendesha kwani Dallas amechukua funguo zote za magari yake.
Ishu hii ikiwa inashika kasi mjini huku watu wakiwa macho juu kutaka kuona nini kinachoendelea kwa
Wolper, Sintah hakusita kudai kuwa mara nyingi mapenzi ya kwenye magazeti huwa hayadumu kwani awali kabisa Wolper alijitangazia kuwa hawawezi kuachana na Dallas huku akisahau kuwa kuna wabaya wake wanaomtazama.
Akiongea na Mpekuzi, Sintah alidai kuwa kwa njisi anavyo mfahamu Wolper
haoni kama yeye atakuwa ndiye chanzo cha kuachana kwao kwani kuna
wabaya wake ambao wamejaa fitna, lakini kwa upande wake anampa pole ili
sasa ajipange na kuacha tabia ya kuishi mjini kwa kuwatengemea wanaume,
hasa wale anaokutana nao mjini.
“Kuachana ni kawaida miaka ya sasa kwanza kama huna hela huwezi
kutembea na staa bongo na Dallas alimpenda Wolper kwa sababu ni staa,
lakini sioni kama kuna tatizo wao kuachana kwani wamekutana mjini na
wanaachana kimjini,”
alidai.