
Nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini Ommy Dimpoz amesema kuwa
licha ya kutumia kiasi cha shilingi milioni 5 kurudisha gari yake
kwenye hali ya kawaida hawezi kumchukia msanii mwenzake Lord Eyez
anayeshikiliwa korokoroni hivi sasa kwa tuhuma za kuiba vifaa kutoka
kwenye gari yake.
Akizungumza na mtandao huu
mapema leo Ommy Dimpoz amefunguka kuwa ingawa kwa sasa haruhusiwi
kusema lolote kuhusu jambo hilo lakini anayo haki ya kusema kuwa
binafsi amesamehe na anamuachia Mungu.
“Nafahamu kuwa kuwa siruhusiwi kuzungumza lolote kwa kuwa suala liko
Polisi,ninachoweza kukwambia ni kuwa binafsi nimemsamehe Lord na
wenzake, sababu huwezi kujua kuhusu kesho, nimepanga kukutana naye na
kumwambia hili jambo, najisikia vibaya lakini nashukuru kuwa gari yangu
nimeshairekebisha na sasa ndiyo ninayoitumia tena licha ya kuwa
nimetumiagharama kubwa” alisema Dimpoz.
Katika hatua nyingine nyota huyo wa songi la ‘Badae’ ameanika kuwa
wimbo huo umemuingizia kiasi kikubwa cha pesa tofauti na yalivyokuwa
matarajio yake huku pia akijikusanyia wingi wa marafiki ndani na nje ya
nchi kupitia wimbo huo.