Aliyewahi kuwa mwakilishi wa Tanzania katika shindano la Big Brother
Africa, 2011, Bhoke Egina ameteuliwa kuwa balozi mpya wa Tanzania wa
taasisi ya Ahadi Trust Tanzania.
Bhoke alikuwa akisherehea siku yake ya kuzaliwa weekend iliyopita na
kuitumia pamoja na rafiki zake kutumia siku hiyo kampeni dhidi ya funza
wa miguuni.
Hafla hiyo ilihudhuria pia na mshindi wa BBA mwaka 2007, Richard
Bezuidenhout.Bhoke alikuwa ni miongoni wa washiriki wa mwaka 2011 wa BBA
walioenda Thika nchini Kenya kuwasaidia watoto walioathiriwa na funza
ambapo anasema hakulijua tatizo hilo mpaka alipowaona watoto hao.
Mguu ulioathiriwa na funza
Tukio hilo lilifanyika mjini Moshi ambapo mwenyekiti mtendaji wa
Ahadi Kenya , Stanley Kamau alimtangaza Bhoke kama balozi wa Tanzania na
kuonesha kufurahishwa kwake na mastaa wanaoguswa na kuhudumia jamii
hasa katika mapambano dhidi ya funza ambao ni tatizo barani Afrika.