Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bwana Seith Kamuhanda
akikagua moja ya majengo ya Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) alipofanya
ziara ya ukaguzi wa Ofisi hizo mpya zilizopo Kijitonyama Jijini Dar es Salaam.Anaemuelekeza
kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Bakita Dkt. Selemani Sewangi.
Baadhi
ya watumishi wa Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) wakimsikiliza Katibu Mkuu
wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo (hayupo pichani) alipofanya
ziara ya ukaguzi wa Ofisi hizo mpya zilizopo Kijitonyama Jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bwana Seith Kamuhanda
akiongea na watumishi wa Baraza la Kiswahili Tanzania (hawapo pichani)
alipofanya ziara ya ukaguzi wa Ofisi hizo mpya zilizopo maeneo ya Kijitonyama
Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa BAKITA Dkt. Seleman
Sewangi na kulia ni Mkurugenzi wa
Maendeleo ya Utamaduni Profesa Hermas Mwansoko
(Picha na Benjamin Sawe wa WHVUM).