MCHAMBUZI: IMORI MARK
MATOKEO
YA DARASA LA 7 NI KITUKO NA NI AIBU KWA TAIFA TOFAUTI NA
ILIVYOWAKILIWASHWA KWENYE VYOMBO VYA HABARI NA WAZIRI HUSIKA.
WAZIRI
ALISEMA IDADI YA WALIOENDA SEKONDARI IMEONGEZEKA UKILINGANISHA NA MWAKA
JANA LAKANA JE WAJUA UFAULU WAO???
------------------------------------------------------------------
WALIOPATA:
A - 3,087,
B - 40,683, C - 222,103
CHUKUA A+B+C = 265,873
WALIOCHAGULIWA KWENDA KIDATO CHA KWANZA NI 560,706.
KWA HIYO WATAHINIWA 294,833 WAMECHAGULIWA KUTOKA DARAJA "D".......WAKATI
DARAJA LA UFAULU KWENDA SEKONDARI NI KUANZIA "C" ....YAANI ALAMA 101/250.
ZAIDI YA 51% YA WALIOCHAGULIWA NI KUTOKA DARAJA "D" YAAN CHINI YA ALAMA 100/250.
JE, KTK HAWA 294,833 TUTAKOSA WASIOJUA KUSOMA NA KUANDIKA VIZURI?
--------------------------------------------------
UPDATE:
Mroki Mroki aka Father Kidevu wa mrokim blog anasema:
"Taarifa zinasema kuwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
inawataka Wazazi, Walezi na wanafunzi kufika katika Ofisi za Elimu Mkoa
au Wilaya zao ndipo majina ya Wanafunzi na Shule walizopangiwa
yanapatikana.