"MBWA WANGU HUNIONDOLEA MAWAZO NA KUNIFARIJI"....JOHARI


STAA wa filamu za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’ amesema kuwa anapokuwa nyumbani kwao marafiki zake wakubwa ni mbwa wake wawili ambao anawafuga kwa sasa.


Akiongea  kwa kujiamini, Johari  alisema kuwa mbwa hao huwa wanamsaidia pindi anapokuwa na mawazo kwani humchangamsha pale anapocheza nao.


“Unajua nawapenda sana mbwa wangu na sijui ni kwa nini nilichelewa sana kuwatafuta, mara nyingi hunifariji wakati ninapokuwa na mawazo mabaya,” alisema Johari. 


Mbali na mbwa hao, pia Johari alisema kuwa  siku mojamoja huenda kuchungulia katika bendi mbalimbali za burudani kwa ajili ya kuchangamsha akili yake.A