
Najma alifanya mazungumzo ya dakika kadhaa na mwandishi wetu maeneo ya Coco Beach, ndipo alipoweka usawa juu ya ishu hiyo, ambapo alisema kuwa hata ishu iliyokuwa inadaiwa kuwa anataka kumvisha pete ni uzushi.
“Suala la mimi na Diamond kuonana studio na kufanya kazi basi limekuwa ishu mtaani, jamani sina mahusiano na msanii huyo na wala simjui kwa chochote zaidi ya msanii tu,” alisema.