NINI
tafsiri ya uelekeo wa dunia kutokana na matukio ya kutisha? Upo
ukatili mkubwa umefanyika nchini Nigeria ambapo mume amemwagia mkewe
mafuta ya petroli na kumchoma moto.
Janet Udegba.
Kehinde Adesamuye, 39, mkazi wa Lagos, Nigeria anadaiwa kumchoma kwa moto wa petroli hivi karibuni mkewe Janet Udegba, 35, katika Mtaa wa Ikotun jijini Lagos baada ya kuwa na hasira kutokana na kuhisi kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na mwanamume mwingine.
Janet alisema wakati wa tukio hilo, alikuwa katika eneo lake la biashara akiuza vyakula kabla ya Kehinde kufika hapo usiku huo na kumwagia petroli mgongoni kisha kuwasha moto kwa kutumia kibiriti.
Janet na Kehinde.
Hata hivyo, alisema Wanigeria hawatamwachia huru Kehinde kutokana na kile alichokifanya. Akisimulia mgogoro wao, anasema:“Mume wangu amekuwa na wivu daima. Amekuwa na tabia ya kunipiga kila wakati. Nimejaribu mara nyingi kuachana naye lakini huwa ananitishia kuwa lazima atanidhuru.
Niliendelea kuishi naye kwa kuwa nilikuwa na
hofu ya maisha yangu, aliwahi kuniambia kuwa sitaweza kutoroka hata
siku moja.
Janet.
“Serikali
lazima ihakikishe kuwa Kehinde analipa kwa kile alichonifanyia. Mimi
ni yatima, ninafanya biashara ya vyakula ili niishi. Sasa nimetumia
pesa zangu zote kwa ajili ya matibabu. Kwa kweli kwa sasa nahitaji
msaada,” alisema mama huyo huku akitokwa machozi.Kehinde alijaribu kutuma rafiki zake ili wamwombee msamaha kwa Janet lakini alikataa. Mtuhumiwa huyo anashikiliwa na polisi kwa ajili ya kujibu mashtaka yanayomkabili.