Mshindi wa shindano la Epic Bongo Star Search 2012/13 Walter Chilambo pamoja na washiriki wenzake waliofika hatua ya kumi bora jana walimalizia tour yao kwa kufanya shoo kali katika ukumbi wa New Maisha Club wakisindikizwa pia na baadhi ya mastaa wa Bongo Flava.
Shoo hiyo ambayo iliandaliwa mahsusi kabisa kutambulisha nyimbo za washiriki ambazo wamezifanya wao binafsi ilianza majira ya saa saba usiku kwa msaanii aliyefanya vizuri kwa mwaka jana Rich Mavoko kufungua shoo na kukonga nyoyo kabla ya wasanii, Linah, Barnaba na Ben Pol hawajawapa sapoti na kunogesha usku huo.
Kwa ujumla wasanii wote wa Epiq Bongo Star Search walijitahidi sana kutawala steji pamoja na kuimba ambapo msanii wababa, Nsami, Husna, menina, Nshoma na Walter Chilambo walikonga nyoyo za wapenzi wa muziki waliojitokeza kushuhudia wasanii hao.
Angalia picha za shoo hiyo pamoja na video ambazo zinapatikana kwenye link ya video hapo chini
Walter Chilambo
Menina Nshoma Husna Barnaba na Sundy Gaga Wababa