MAKAMUZI YA DIAMONDI,BARNABA,ALLY KIBA JIJINI DODOMA



Msanii wa kizazi kipya Diamond akiwa ameinuliwa juu na madansa wake katika onyesho la ziara ya washindi wa tuzo za muziki za Kilimanjaro lililofanyika juzi Jumamosi kwenye Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma.


 
Madansa wa mwimbaji Ommy Dimpoz wakiweka mlango kwa ajili ya msanii huyo kupita ili kuweza kuwapa burudani wakazi wa Dodoma wakati wa onyesho la washindi wa tuzo za muziki za Kilimanjaro lililofanyika juzi kwenye Uwanja wa Jamhuri.

 
Barnaba akiwabembeleza mashabiki wa wa muziki wa Bongo Fleva Mjini Dodoma katika onyesho la vinara wa tuzo za muziki za Kilimanjaro lililofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa mpira wa miguu Jamhuri.

 
Nyota wa muziki wa kizazi kipya Ally Kiba, akitoa burudani pamoja na madansa wake kwenye Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma juzi Jumamosi wakati wa onyesho la washindi wa tuzo za Kilimanjaro


Mashabiki waliofika kwenye Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma kufutilia onyesho la vinara wa tuzo za muziki za Kilimanjaro, ambalo lilifanyika mwishoni mwa wiki.