Mama Lulu Avunja Ukimya - 'Msimhukumu Mwanangu Muuaji'



Mama mzazi wa msanii Elizabeth Michael au maarufu kwa jina la Lulu amevunjika ukimya na kuwaomba watanzania wasimhukumu mwanae kama muuaji wa msanii Steven Kanumba na badala yake wavute subira ukweli utajulikana tu.

Mama mzazi wa Lulu ambaye bado anaendelea kushikiliwa na polisi kuhusiana na kifo cha msanii Steven Kanumba aliyefariki usiku wa kuamkia jumamosi iliyopita, amejitokeza baada ya mazishi ya Kanumba na kuwaomba Watanzania waache kumhukumu binti yake kuwa ni muuaji wa Kanumba.

Mama Lulu alisema kuwa Kanumba ni kama mwanae kwakuwa alikuwa akimuita mama na pia Lulu ni binti yake hivyo anawaomba Watanzania wavute subira ukweli utajulikana tu na wala wasimhukumu mwanae kuwa ndiye aliyemuua Kanumba.


Mama Kanumba pia ameelezea kusikitishwa kwake na kifo cha Kanumba na ameomba msaada wa wanasheria kutetea haki za binti yake Lulu.