MIMBA YA SAUDA INATAKA MUMEWE ASHINDE NDANI


MIMBA ya Mtangazaji wa Kituo cha Star Tv, Sauda Mwilima imegeuka kuwa ya maajabu baada ya hivi karibuni kukiri kuwa kila wakati anataka kuwa karibu na mumewe, Kauli Juma.

Akiimegea Za Motomoto Newz, Sauda aliweka kweupe kuwa anamshukuru Mungu mimba yake inapenda kila kitu, haichagui chakula wala vinywaji ila kinachomkosesha amani ni pale mumewe anapokuwa mbali kwani hushindwa hata kula kutokana na penzi la dhati alilonalo kwake.
“Katika kipindi hiki cha ujauzito, ninampenda sana mume wangu kuliko kitu kingine, natamani kila wakati niwe naye karibu, nikiwa naye mbali nashindwa kula,” alisema Sauda.