Baada ya
kusumbuliwa kwa kipindi kirefu kwa ugonjwa ambao ulisababishwa na uvimbe
tumboni hatimaye mwigizaji machachari kabisa kunakoulingo wa filamu
hapa nchini Juma Kilowoko maarufu kwa jina la Sajuki amerejea nchini
siku kadhaa zilizopita. Akiwa anazungumza na waandishi wa
Globalpublishers Sajuki alidai kwa sasa hali yake imerejea kama zamani
na anawashukuru Watanzania wote waliomchangia kwa hali na mali
kufanikisha matibabu yake na anathamini mchango wao, bila kuwafumbia
macho waliokuwa wanazungumza yasiyokuwepo Sajuki hakuacha kuzungumzia
waliomzushia kifo na kusema kuwa yeye hana kinyongo na
mtu na Mungu awabariki. Pichani ni sajuki baada ya kurejea kutoka India alikokwenda kwa matibabu.