Je! Unafahamu kuwa Saraha alishawahi kuishi Tabora akiwa na miaka miwili?


Bila shaka umeshamsikia mwanadada raia wa Sweden Saraha Msanii akiimba nyimbo kwa Kiswahili fasaha na kujiuliza amekijuaje.

Akiongea na kipindi cha Popote Afrika cha Sibuka TV, Saraha ambaye kwa sasa ameachia wimbo mpya uitwao ’Jambazi’ alisema amewahi kuishi Tanzania akiwa mdogo kabisa kabla ya kurudi tena kwao Sweden.
Akiwa na miaka miwili tu, alikuja Tanzania akiwa na wazazi wake na waliishi mkoani Tabora ambako baba yake alikuwa akifanya kazi huko.
Baadaye alirejea Sweden alipokuwa na miaka mitano hivyo aliweza kuongea Kiswahili alipokuwa mtoto mdogo lakini baada ya kukaa kwa muda mrefu Sweden alisahau kabisa Kiswahili lakini aliikumbuka sana Tanzania.
Baada ya kufunga ndoa na mume wake Fundi Samweli ambaye ni producer wa Usanii Production miaka sita iliyopita alipenda kumleta Tanzania kwaajili ya honey moon ili amwoneshe palivyo.
Walipokuja Tanzania walitembelea marafiki wa zamani sana na kujikuta yeye na mume wake wakiipenda tena Tanzania.
Anasema siku anafika Tanzania aliweza kusikia kwa mara ya kwanza wimbo wa Ali Kiba Cinderella ambao aliuskiliza kwa muda mrefu na kuupenda sana.Baadaa hapo alianza kufanya utafiti zaidi juu ya Bongo Flava kwa kusikiliza wasanii wengi zaidi ili kuujua muziki huo na hatimaye naye kuanza kuimba.
Hata hivyo aliongeza kuwa muziki wa Tanzania ni mgumu kwakuwa biashara ya kanda za muziki na CD ni kama imekufa kutokana na wizi wa kazi za wasanii uliokithiri na pia ni mgumu kwakuwa hapa nchini hakuna utaratibu wa wasanii kulipwa fedha kutokana na kuchezwa kwa nyimbo zao redioni tofauti na nchi zilizoendelea kama Sweden na hivyo wasanii kubaki kutegemea show peke yake ambazo nazo hazipo mara kwa mara.
Kuhusu show za wasanii wa Tanzania, alisema nyingi zina ubora wa hali ya chini ambao huchangiwa kwa kiasi kikubwa na vifaa duni na sound system mbaya, hivyo hufanya show ya live kuwa ngumu na ndo maana wasanii wengi hupendelea kufanya playback.
Kwa sasa anafanya collabo na Marlow ambaye anamsifia kuwa na sauti ya pekee na anamchukulia kama mwimbaji bora kabisa nchini. Albam yake iko mbioni kukamilika na tayari nyimbo saba zimeshakamilika.