Blandina Chagula ‘Johari’.
STAA wa kitambo ndani ya Bongo Movie, Blandina Chagula ‘Johari’ amefunguka kuwa Msanii Elizabeth Michael ‘Lulu’ aliangukiwa na jumba bovu hadi kuhusishwa na kifo cha marehemu Steven Kanumba hivyo anatakiwa kuwa na moyo wa uvumilivu.
Akifafanua kauli yake, Johari alisema, kifo kinaweza kumtokea mtu yeyote na wakati wowote na kwa kuwa kilimtokea Kanumba akiwa na Lulu siku hiyo, basi ndiyo hivyo msala umemuangukia.
“Marehemu alishatembea na mastaa kibao kabla hata ya Lulu lakini maskini kifo kikatokea akiwa naye. Kwa kweli namuonea huruma sana japo sina jinsi ya kufanya, kikubwa awe na moyo wa uvumilivu na amuombe Mungu,” alisema Johari.
Hata hivyo, msanii huyo amesema kuwa, anaamini mahakama ni chombo cha kutenda haki hivyo siku moja Lulu atarejea uraiani kuendelea na shughuli zake za kisanii.