Yanga Bingwa Kagame Cup, Yaichapa Azam 2-0

Kipre Cheche kulia Mchezaji wa timu ya Azam FC akikokota mpira mbelea ya beki wa Yanga Nidir Haroub Canavaro wakati wa mchezo wa fainali ya kombe la Kagame inayofanyika kwenye uwanja wa Taifa jioni hii, mpira umekwisha na timu ya Yanga imefanikiwa kutetea kombe la Kagame kwa mara ya pili mfululizo baada ya kuitandika timu ya Azam FC goli 2-0 jioni hii.

Mashabiki wa timu ya Yanga wakishangilia mara baada ya timu yao kupata goli la kuongoza katika mchezo huo.


Timu zikiingia uwanjani kuanza mpambano huo.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam akielekea kukagua timu kabla ya mchezo huo kuanza kulia ni , Crecentius Magori kushoto Makamu Mwenyekiti wa timu ya Yanga Clement Sanga na katikati ni Mwenyekiti wa Azam FC mzee Mohamed Sai.

Magoli mawili yaliyopachikwa wavuni na washambuliaji wa Yanga Hamisi Kiiza katika dakika ya 44 kipindi cha kwanza na lile la Said Bahanuzi katika dakika ya 90 ya mchezo yameiwezesha Yanga kuibuka Mabingwa tena wa Kombe la Kagame 2012 baada ya kuchapa bila huruma mahasimu wao Azam FC kwa goli 2-0, katika mchezo wa fainali uliochezwa leo katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Tanzania ijnakila sababu ya kujivunia ushindi huo wa Yanga na nafasi ya pili ya Azam katika michuano hiyo ya mwaka huu ambapo Tanzania kama mwenyeji wa michuani huyo iliingiza timu 4 zikiwapo za Simba na Mafunzo zilizotolewa katika hatua ya robo fainali.

Yanga pia waliutumia mchezo wa leo kulipiza kisasi cha kufungwa goli 3-1 na Azam katika mchezo wao wa Ligi Kuu msimu uliopita na kupelekea wachezaji kadhaa wa Yanga kufungiwa baada ya kushambulia mwamuzi kwa ngumi.