Marais wa Tanzania na Malawi wakutana Msumbiji

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Malawi Mhe.Joyce Banda mjini Maputo Msumbiji walipokutana leo asubuhi kuzungumzia kutafuta suluhu katika mgogoro wa mpaka kati nchi hizo uliopo kwenye ziwa Nyasa.Wakati wa mazungumzo hayo Marais hao wawili wameelezea nia ya nchi zao kufikia suluhu kwa njia za kidiplomasia kupititia kamati maalumu iliyoundwa kushughulikia mgogoro huo  (picha na Freddy Maro).
Rais wa Malawi Mhe.Joyce Banda akisalimiana na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete mapema leo asubuhi mjini Maputo Msumbiji,walipokutana  kuzungumzia kutafuta suluhu katika mgogoro wa mpaka kati nchi hizo uliopo kwenye ziwa Nyasa.Wakati wa mazungumzo hayo Marais hao wawili wameelezea nia ya nchi zao kufikia suluhu kwa njia za kidiplomasia kupititia kamati maalumu iliyoundwa kushughulikia mgogoro huo.
 Marais wakizungumza kwa furaha kabisa.
Rais Dkt.Jakaya Kikwete akifafanua jambo mbele ya Wanahabari mapema leo asubuhi mjini Msumbiji,ambapo Rais Kikwete amekutana na Rais wa Malawi Mhe.Joyce Banda kuzungumzia kutafuta suluhu katika mgogoro wa mpaka kati nchi hizo uliopo kwenye ziwa Nyasa.Wakati wa mazungumzo hayo Marais hao wawili wameelezea nia ya nchi zao kufikia suluhu kwa njia za kidiplomasia kupititia kamati maalumu iliyoundwa kushughulikia mgogoro huo.