UJIO WA JASMIN HUENDA UKAMPOTEZA JACK WOLPER KATIKA SANAA YA MAIGIZO

MWIGIZAJI wa kike anayekuja kwa kasi katika tasnia ya filamu Neema Oberlin Kimaro ‘Jasmin’ uenda akawa tishio kwa msanii anayeng,ara kwa sasa katika tasnia ya filamu ambaye ni Jaqueline Wolper Massawe.

Neema mbali ya kuwa ni msanii anayetoka Mkoani Kilimanjaro anakotoka mpinzani wake Jack kwa muda mfupi toka aingie katika tasnia ya filamu ameonyesha uwezo mkubwa baada ya kushiriki filamu ya Essau Hellen akiwa mhusika mkuu katika filamu hiyo.


Neema Oberlin Kimaro.

“Toka nianze kuigiza filamu zote watayarishaji wamekuwa wakinikubali na kusema kuwa mimi uwezo wangu ni mkubwa na ninaweza kabisa kumpoteza dada yangu Jack ambaye pia kwangu ni moja kati ya wasanii wanaonivutia sana yeye na wasanii kama Monalisa na Johari kupitia kazi zao walizofanya...

 nipo kikazi zaidi na sihofii ushindani bali siku ya siku mimi ndio natarajia kuwa mshindi katika tasnia ya filamu Bongo,”anaongea huku akicheka Neema.

Mtayarishaji wa filamu hiyo Mshindo Jumanne anasema kuwa amekuwa mara nyingi akiibua vipaji kwa wasanii wake lakini huyu ameonyesha uwezo wa hali ya juu sana.


Filamu ya Essau Hellen imeandaliwa na SSG Distributors . Jasmini  amecheza kama mhusika mkuu akiigiza kwa kutumia jina la Jasmin nafasi ambayo imechezwa na wahusika wawili yeye na msanii mkongwe Grace Mapunda (Mama Kawele).


Kutokana na mgawanyo wa umri msanii huyo amejinasibu kuwa watanzania watarajie makubwa kutoka kwake hususani katika filamu hii ya Essau Hellen ambayo ameshirikiana vyema na wakongwe kama Mohammed Fungafunga ‘Jengua’, Fadhili Msisiri ‘Mzee Msisiri’ na Grace Mapunda ‘Mama Kawele’.