Baada
ya Mweyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dk.Steven Ulimboka,
kurejea nchini kutoka afrika Kusini alikokuwa anatibiwa, hali ya ulinzi
imezidi kuimarishwa nyumbani kwa wazazi wake alipofikia.Hali hiyo
ilitokana na watu mbalimbali kujitokeza kwa wingi nyumbani kwa wazazi
wake jana kumjulia hali Dk. Ulimboka na kuzuiliwa kuingia ndani kumuona.
Hali
ya nyumbani kwa wazazi wake ilikuwa imebadilika tofauti na hapo awali
baada ya kufungwa kwa geti kubwa katika mlango mkubwa wa kuingia
nyumbani.
Awali
kulikuwepo na ukuta ambao haukuwa na geti, huku baadhi ya watu wakisema
ni kwa ajili ya usalama.Nje ya nyumba hiyo kulikuwepo na vijana
waliokuwa wakiwafuatilia watu wote waliokuwa wakifika.
Paparazzi
walifika nyumbani Ubungi Kibangi na kukuta umati mkubwa wa watu wakiwa
ndani na nje ya nyumba hiyo kumjulia hali Dk. Ulimboka.
Kufuatia
hali hiyo, Paparazzi walijaribu kuzungumza na baadhi ya watu waliofika
nyumbani hapo akiwemo mama mzazi wa Dk, Ulimboka ambapo hakuwa tayari
kuzungumza.
Baada
ya waandishi kujitambulisha, baba mzazi aliwaamuru kuondoka eneo hilo
kwa maelezo kuwa wanaotakiwa kufika hapo nyumbani ni ndugu na si watu
wengine.
Tangu
kutekwa, kuteswa kwa kupewa kipigo kwa Dk. Ulimboka, wazazi wake
wamekuwa na wasiwasi na watu mbalimbali waliokuwa wakijitokeza kufika
nyumbani kwao kuwafariji kwa tukio lililomkuta kijana wao.
Dk.
Ulimboka alitekwa, kuteswa na kupata kipigo Juni 26, mwaka huu na watu
wasiojulikana na kutelekezwa katika msitu wa Mabwepande na kuokolewa na
msamaria mwema kisha kupelekwa katika Taasisi ya Mifupa (MOI) kabla ya
kupelekwa Afrika Kusini kwa matibabu zaidi.
Chanzo: http://www.kwetubongo.com