ALICHOSEMA PRODUCER MANECK BAADA YA KUONA DOGO JANJA ANATAKA KUMGOMBANISHA NA MARCO CHALI.

Producer
Maneck ambae ni mshindi wa tuzo kwenye KTMA 2012 ameamua kuzungumza ya
moyoni kwa kuijibu kauli Dogo Janja aliyoitoa kwamba Producer huyo
kauponda uwezo wa Marco Chali.Ishu ilianza wakiwa club Maisha Dar
es salaam jumapili iliyopita ambapo Dogo Janja anadai alikwenda sehemu
ya V.I.P na kumsalimia Maneck ambae hakujibu salamu ila aliporomosha
matusi mazito kwa Dogo Janja pamoja na kumpiga biti kwamba asimsogelee.
Baada ya hapo Dogo Janja akashuka
chini kwenda kumwita meneja wake wa WATANASHATI ambae ni Ustaz Juma
ambapo kwa maelezo ya Dogo Janja, Maneck alianza kuiponda single mpya
ya Dogo Janja na PNC waliyoirekodi kwa Marco Chali ambayo mwanzoni
ilikua irekodiwe kwa Maneck alieiponda kwa kusema ni ya kawaida sana kwa
sababu imefanywa na Marco Chali.
Jibu alilolitoa Maneck baada ya
kusikia kwamba Dogo Janja amenukuliwa kwa hayo maneno, namkariri
akisema “ndio ninavyokwambia sitakagi watu masnich kama huyo, Marco
Chali ni mtu ambae namfil sana anafanya kazi nzuri, siwezi kuongea kitu
kibaya kwa Marco kwa sababu leo na kesho nitamfata nitamuomba msaada wa
kitu chochote kile hata material sasa nitawezaji kusema hivyo kwa
mfano sasa, Dogo Janja ni mtu ambae anataka tu kufanyaga vitu watu
wapishane kauli mambo ya kijinga ni utoto akikua nadhani ataacha hizo
tabia zake, na ndio maana nikamwambia kaa mbali sitaki uongee na mimi
that’s all”