
MSANII
wa Mziki wa Kizazi kipya anaetamba na nyimbo zake mbili za Nai Nai na
Badaye, na mshindi wa Tuzo mbili za Kili Music Award 2012, Omy Dimpoz
anataraji kuzindua Video yake mpya ya Baadaye katika ukumbi wa Club
Maisha Septemba 9,2012 jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na Father Kidevu Blog, Meneja wa Msanii huyo, Mbaruku Issa ‘Mubenga’
alisema kuwa maandalizi yote yamekamilika na show itakuwa ya uhakika
naya kuvutia.
Mubenga amesema Omy Dimpozy ameifanyia shooting video yake hiyo nchini Afrika Kusini.
Aidha
Mubenga amesema kuwa kazi ya utayarishaji wa vuideo hiyo ulifwanywa na
Adam Juma wa Visual Lab ambaye ndiye walisafiri nae hadi Afriia
Kusini na wameshoot kwenye
maeneo mazuri na ya kifahari yaliyopo nchini humo ambapo ameona
utofauti mkubwa katika kufanya video nje na nyumbani.
“Kazi hii ni ya uhakika ambayo tunaizidua Jumapili hii na Video hiyo imefanyika Johannesburg mitaa ya Sendton na nikatika location kali na za uhakika,”alisema Mubenga.
Amesema
wasanii kadhaa watasindikiza uzinduzi huo akiwepo Chegge Chigunda,
Suma Mnazareth na Nas 3 siku hiyo katika uzinduzi wa video hiyo mpya
na Dimpoz nae atakuwa katika muonekano tofauti si Dimpoz waliye mzoea.
Pia
Meneja huyo wa Omy Dimpoz amesema akiwa nchini Afrika kusini Dimpoz
alimshirikisha Model ambaye amekuwa akifanya kazi na wasanii wengi
wakali wa Mziki nchini humo anaejulikana kwa jina la Tully Tshabalala.
“Wimbo
ni mkali na mashabiki wanaukubali vilivyo na tunaomba mashabiki wa
Bongo Fleva wakae tayari kwa video hiyo mpya itakayoanza sasa kuchezwa
katika vituo vya Televisheni nchini na kumbi za burudani baada ya
uzinduzi huo,” alisema Mubenga.
Mubenga
amewakata wakazi wa jiji la Dar es Salaam ambao ni mashabiki na
wapenzi wa muziki wa kizazi kipya kujitokeza kwa wingi kumpa support
Dimpoz katika uzinduzi huo wa aina yake katika Club Maisha Oyster bay
jijini la Dar es Salaam jumapili.