Heka Heka za Maisha Plus zimeanza

Usaili wa Maisha Plus 2012 waendeleaUsaili wa Maisha Plus umeendelea leo (Septemba 4) mkoani Mwanza; baadaya hapa timu nzima itaelekea Morogoro katika wilaya ya Mvomero na siku inayofuata itaibukia Igula, Mkoani Iringa.
"Tukitoka Iringa tunahamia Sumbawanga huko Kantalamba then tutarudi Mbeya, baadaye tutaelekea Kilwa kisha Masasi na Zanzibar itafuatia.

Dar es Salaam itakuwa ya mwisho ambayo usaili wake utafanyika Septemba 22 na 23," anasema Masoud Kipanya.

Fomu za kushiriki shindano hili kwa Dar es Salaam zinapatikana katika Duka la KP lililopo Millenium Towers Kijitonyama. Kama unahitaji fomu piga namba 0717104303 uelekezwe.

Kaka Bonda akihoji  vijana juu ya Maisha Plus
Masud Kipanha akiongea na Mama Shujaa akionesha ushaa wa chakula