Makamu
Waziri mkuu wa China Hui Liangyu akiwapungia mkono Viongozi mbalimbali
waliokuja kumpokea baada ya kuwasili Zanzibar hapo jana kwa Ziara ya
Siku mbili.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi wakwanza kushoto akiwa
na mgeni wake Makamu Waziri Mkuu wa China Hui Liangyu wakatikati baada
ya kuwasili Zanzibar hapo jana.mwengine ni Balozi mdogo wa China
alioko Zanzibar Bibi Chen.
Rais
wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein wakwanza kulia amekutana na kufanya
mazungumzo na Makamu waziri Mkuu wa China Hui Liangyu wamwisho kushoto
baada ya kufika Ikulu Mjini Zanzibar.
Waziri
wa Nchi Afisi ya Rais Fedha na Mipango ya Maendeleo Omar Yussuf Mzee
akibadilishana mafail na Naibu Waziri wa Biashara wa China Zhong Shan
baada ya kutiliana saini kuhusu mashirikiano yaKiuchumi na kimaendeleo
kati ya Zanzibar na China .
Viongozi
mbalimbali kati ya Zanzibar na China wakihudhuria katika Chakula cha
Usiku kilichoandaliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif
Ali Idi huko katika Hoteli ya Lagema ilioko Nungwi kaskazini Unguja.
Makamu
wa Pili wa Rasi wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi wakatikati akipiga
makofi pamoja na Mgeni wake katika Muziki uliotumbuizwa na Kikundi cha
Taarab cha Tausi katika Hoteli ya Lagema ilioko Nungwi kaskazini
Unguja.
PICHA NA YUSSUF SIMAI MAELEZO ZANZIBAR
|
|