SIKU
chache baada ya kuanika utajiri wake, staa wa Bongo Movies, Wema Isaac
Sepetu (pichani), amevamiwa na majambazi na kukombewa vitu kadhaa huku
gari lake aina ya Toyota Lexus lenye namba za ujsali T 211 BXR
likinusurika kuibwa, Ijumaa lina kila sababu ya kukujuza.
Tukio
hilo lilijiri usiku wa kuamkia Julai 9, mwaka huu, nyumbani kwake
Kijitonyama, jijini Dar es Salaam ambapo majambazi hayo yaliingia ndani
kwake kwa kuruka ukuta licha ya kwamba kuna walinzi wawili.
KIKWAZO CHA NGUVU
Hata
hivyo, baada ya kuzamia ndani ya geti, majambazi hayo yalishindwa
kuingia ndani kabisa kutokana na milango madhubuti iliyopo kwenye nyumba
hiyo ya kisasa.
WAJIPOZA KIDOGO
Kule ndani ya geti, walivunja mlango wa gari hilo na kuiba
vitu
mbalimbali kama kifaa cha kudhibiti mwenendo wa umeme ndani ya gari
(control box), vifaa vya kufungulia vioo, milango na madirisha (power
window) na vioo vinavyomuongoza dereva kuona nyuma (side miller). Vitu
vingine ambavyo viliambatana na wizi huo ni ‘makapeti’ ya ndani na
vitu vingine vidogovidogo ambavyo vilikuwa ndani ya geti hilo.
WEMA AWASHANGAA WALINZI WAKE
Akielezea
mazingira ya tukio hilo, Wema alisema kuwa hata yeye ameshangazwa na
uvamizi huo ambao umemfanya kuibua maswali mengi kuliko majibu hasa
akizingatia kuwa tukio hilo limetokea wakati nyumba yake ina walinzi
wawili.
“Ni
kweli nimeibiwa hivyo vitu kwenye gari na vingine vilikuwa nje, ila
mazingira ya kuvamiwa na yale majambazi yananitia shaka sana maana
walinzi wangu wawili walikuwepo muda wote, sasa sijui nini kilitokea?”
alisema Wema kwa sauti ya kupooza.
Akaendelea:
“Sikuwa na namna kwao, nilikwenda kutoa taarifa katika Kituo cha
Polisi Oysterbay ili angalau nisaidiwe utatuzi wa jambo hili sambamba
na kuwabananisha walinzi wangu ambao walikuwepo usiku wa tukio.
“Naamini
kama geti la kutokea nje lingekuwa legelege, wangeiba na gari lenyewe.
Lakini hili geti ni gumu, mpaka kulifanya lifunguke wangeweza kuchukua
masaa matano ambapo kungekuwa kumekucha.”
INAWEZEKANA SABABU IKAWA HII?
Katikati
ya Juni mwaka huu, staa huyo ambaye pia ni Miss Tanzania 2006,
alitangaza kupitia runinga kwamba anamiliki nyumba hiyo huku akisema ina
kila kitu ndani.
Kwa
mujibu wa picha zilizoenea kwenye mitandao mbalimbali Bongo, sebule ya
nyumba hiyo inaweza kushawishi ‘wazee wa kazi’ kunyatia kwani Meneja
wa Wema, Martin Kadinda alisema manunuzi ya nyumba hiyo pamoja na
samani zake shilingi Milioni 4OO ‘ziliteketea’.
HABARI ZA KIPOLISI ZATHIBITISHA
Kamanda
wa Mkoa wa Kipolisi, Kinondoni, Charles Kenyera hakupatikana siku ya
Jumanne kuzungumzia tukio hilo licha ya kwamba, habari za kipolisi
zilithibitisha Wema kukumbwa na uvamizi wa watu wanaodhaniwa ni
majambazi.
Na Musa Mateja (Global Publishers)