Internet ni maktaba kubwa ambayo maandishi, muziki, video na picha zikishasambaa huwezi kuvifuta daima.
Na
ndio maana picha maarufu ya mfalme wa rhymes Seleman Msindi aka Afande
Sele inayomwonesha akirap jukwaani akiwa kifua wazi na kuvua suruali
huku akibaki na ‘boxer’ nyeusi imeendelea kuwa jinamizi linalomrudia
kila kukicha.
Na
sasa kwakuwa rapper huyo aliyepotea kwenye playlist ya radio nyingi
Tanzania ametangaza nia ya kugombea nafasi ya kubwa kwenye uchaguzi wa
mwaka 2015, amejikuta katika wakati mgumu baada ya maadui zake kutumia
magazeti ya udaku kumchafua kwa kuitumia picha hiyo.
“Haya magazeti yanakwenda wapi?” alihoji Afande kupitia Clouds FM. “Katika
furaha yangu, mimi siku hiyo ilikuwa ni siku ya birthday ya mtoto
wangu Tunda nikaonesha na mimi bukta yangu ambayo ilikuwa na maandishi
watu wakachukulia kama kawaida.
Lakini
sasa watu ambao hawakupendi ndio wanakuza lolote lionekane baya na sio
ajabu, wiki moja baadaye 50 alikuja akavua akabaki na chupi. Mbona 50
kavua kabaki na chupi watu wanamshangilia?”
“Wanavyoenakana wametumwa. Sio siasa nzuri ni siasa chafu, mapema sana hatuwezi kuikomboa nchi kwa mazingira hayo.
Pengine
labda shida yao mimi nionekane mimi labda ni chizi au ni mwendawazimu
kwahiyo yawekazana watanzania pia wameona sasa hivi wanahitaji viongozi
wendawazimu kama sisi, kwasababu wameshaamini viongozi wenye akili
mpaka leo ni nchi inayoongoza kwa umaskini duniani.
Ina rasilimali kibao lakini hawa wanaoonekana wanavaa masuti na akili nyingi hawajasaidia lolote. Ni bora sisi twende na bukta bungeni lakini tuwe na vitu kichwani vya kuongea.”