
Mmoja
wa wasanii mahiri katika miondoko ya hip hop hapa nchini
akiwaimbisha wakazi wa mji wa Tabora wimbo wake wa Yalaiti,usiku wa
kuamkia leo katika viwanja vya Ally Hassan Mwinyi,ambapo wakazi wa mji
huo walijitokeza kwa wingi.Tamasha hilo jumapili litakuwa linarindima
mjini Singida katika kiota cha marahaa kiitwacho Singida Motel

Anaitwa
Godzilla,Msanii wa hip hop katika muziki wa kizazi kipya,akiangusha
mistari iliyowasisimua mashabiki mbalimbali waliofika kwenye tamasha la
Serengeti Fiesta 2012 usiku wa kuamkia leo kwenye uwanja wa Ally Hassan
Mwinyi,ambapo katika tamasha hilo wakazi wa mji wa Tabora walijitokeza
kwa wingi na kujishuhudia vipaji mbalimbali vya muziki.
