WACHACHE WAHUDHURIA SHOW YA LINAH JIJINI LONDON


Ukweli ndio huu. Unaposikia msanii wa Tanzania ameenda kupiga show nchini Uingereza, usidhani hupata shangwe na nyomi kama alipatalo pale Dar Live! Show za huko ziko tofauti kidogo. 
Ni show za watu wachache tu ambao mara nyingi wako busy kukimbizana na maisha ya ughaibuni lakini huamua kutumia siku moja kuburudika kwa kumshuhudia msanii wa Tanzania.
Weekend hii Linah amepiga show kwenye club jijini London iitwayo Club Solar. Ilikuwa show ya kawaida tu ambapo watu walijikusanya kwa mtindo wa Cocktail kwenye club hiyo na kumzunguka Linah aliyekuwa akitumbuiza. 



Ukitazama picha hizi, watu waliohudhuria ni wachache na wanahesabika. Hawazidi 100 lakini it’s all good kama waliburudika na Linah alipata hela yake safi ya kuweka benki.


Baadhi ya wanaume waliondoka na kitu cha kusimulia nyumbani kwakuwa walipata fursa ya kucheza naye, fursa ambayo wanaume wa huku Bongo hupewa kwa nadra!!

IMG_6171 IMG_6172 IMG_6194 IMG_6195 IMG_6200 IMG_6204 IMG_6205 IMG_6206 IMG_6212 IMG_6213 IMG_6214 IMG_6215 IMG_6219 IMG_6230 junior birthday & Linah4