Askari Polisi Wapewa Zawadi
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Stanslaus Mulongo
akimkabidhi cheti cha utendaji bora wa kazi askari wa Jeshi la Polisi
mkoani humo Mkaguzi Msaidizi wa Polisi (ACP) Jane Warioba wakati wa hafla fupi
iliyofanyika katika uwanja wa michezo uliopo katika kambi ya
polisi ya mjini Arusha tarehe 08/10/2012. (Picha zote na Rashid Nchimbi
wa Jeshi la Polisi Arusha).
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo akikagua
gwaride lililoandaliwa na Jeshi la Polisi mkoani hapa wakati wa hafla ya
kukabidhi vyeti kwa askari 37 wa mkoa huo waliofanya vizuri zaidi
katika utendaji wao wa kazi za kila siku. Hafla hiyo ilifanyika tarehe
08/10/2012 katika uwanja wa michezo uliopo katika moja ya kambi ya
jeshi hilo iliyopo mjini Arusha.
Baadhi ya askari wa Jeshi la Polisi mkoani Arusha wakiwa
katika picha ya pamoja mara baada ya kutunukiwa vyeti na fedha taslimu TSh
100,000 kila mmoja kutokana na utendaji mzuri wa kazi zao za kila
siku.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha (ACP) Liberatus Sabas
akimkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo ili
aweze kutunuku vyeti na fedha taslimu TSh 100,000 kwa kila askari ambaye
alikuwa amefanya vizuri zaidi katika utendaji wake wa kazi za kila siku.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo akisalimiana na
baadhi ya viongozi wa Jeshi la Polisi wa Mkoa huo mara baada ya
kuwasili katika uwanja wa michezo uliopo katika moja ya kambi
zilizopo mkoani humo. Kulia kwake ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha
(ACP) Liberatus Sabas akimtambulisha viongozi hao.