Msanii wa ‘Kiuno’ Khalid Mohamed aka Top In Dar amesema anatamani
aumalize mgogoro wake na waandaaji wa tuzo za Kili baada ya mwaka 2010
kukataa kushirikishwa kwenye tuzo hizo.
“I Really want to finish my differences with Kili Music Awardz so I
can pursue my dream of becoming a better Artist for my Country,”
ameandika leo TID kwenye ukurasa wake wa Facebook.
“Sometimes in life u feel the fight is vver and seemz as tho the
writings is on the wall,Superstarz u finally made bt ur picture become
tainted that is wat they call Rise and Fall-Sting and Craig.”
Baada ya kutajwa kuwania tuzo za Kili mwaka 2010, TID aliandika barua ndefu kuzungumzia sababu za kujitoa kwenye tuzo hizo.
HII NDO BARUA YAKE:
“Naomba radhi kwa mashabiki wangu wote kutoka pande zote za sayari
hii najua mlikua mnasubiria kunipigia kura kwenye hiki kinyanganyiro cha
award hizi za kilimanjaro,najua imekua uamuzi muafaka kwangu kujitoa
kwene awards hizi basi naomba muelewe sababu zangu hizi za msingi:
1.Kwanza nahisi mimi kama TID na mziki ninao perfom kwa kipindi chote
hiki cha miaka saba toka nimepewa tunzo hizi sina umuhimu wa kuwa
shiriki sababu hata nikitengeza wimbo ambao unakubalika sana na wapenzi
wa muziki huu wa kizazi kipya sipewi tuzo kwa mantiki hiyo naona sioni
sababu ya kuwa kwenye tuzo hizi.
2.Pia nilidhani labda ni upungufu wa mawazo ya majaji ama waandaaji
ambao imewezekana nilitofautiana nao kipindi fulani nilipokuwa nafanya
nao kazi za maonesho,inauma sana unapoona wengine ambao uko nao kwenye
same field wanapewa nafasi kubwa ambayo pia mimi nastahili kutokana na
juhudi ambazo nafanya kwenye sanaa hii ya kizazi kipya hapa nahisi
sihitajiki kwani kama wimbo wangu wa bendi ni bora wa mwaka kwanini
nisiwe mwanamuziki bora wa kiume mwaka huo,pia hata video zangu huwa za
viwango vya juu nazo hazipewi nafasi kwenye video bora za mwaka!