Hivi karibuni kumekuwepo na tetesi kuwa muimbaji Khalid Mohamed aka
Top in Dar amecopy wimbo wa Shayman uitwao Fendela Fenduze na kuupa jina la "KIUNO". Tumepata
fursa ya kuzilinganisha nyimbo hizo.
Tofauti na shutuma hizo tumegundua
hakuna mfanano wowote wa nyimbo hizo na kuamua kumpigia simu TID
kumuuliza analizungumziaje suala hilo.
“Mimi naona tu kuna watu ambao wanataka kuniangusha. Kwasababu
wameona muziki wangu unakua vizuri kwahiyo hawataki nipate advantage
wananiharibia lakini ukweli ni kwamba hakuna mtu ambaye amemcopy huyo
jamaa wala simjui toka nilivyozaliwa,amesema TID.
“Sababu mimi sijafanya kosa lolote mimi nitakatu kimya, nitaangalia.”
Hiyo sio mara ya kwanza kwa TID kuzushiwa kucopy wimbo wa msanii
mwingine kwani aliwahi pia kuingia kwenye shutuma ya kucopy wimbo wa
Irmãos Verdades uitwao Amar-te assim ambao kweli ulifanana kwa asilimia
kubwa.