Wanavyuo Wachambua Sera Mbovu Za Serikali UN


 Mtaalam wa Mazingira wa UNDP Bw. Amani Ngusaro akitaja baadhi ya vikwazo vinavyo kwamisha uboreshaji wa Mazingira katika maeneo ya makazi ikiwemo uhaba wa maji na kutaka vikwazo hivyo viangaliwe upya na kuboreshwa sambamba na kutolewa kwa elimu ya Mazingira na uhamasishaji katika ngazi zote


 Afisa Misitu Mkuu katika Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Freddy Manyika akitoa nasaha zake kwa kusema kuwa sisi wananchi ndio tunatakiwa kuwa wa kwanza kufanya mabadiliko na sio kuilaumu serikali kwani ndio tunaozungukwa na mazingira. Aidha pia ametumia nafasi hiyo kutangaza kuwa suala la mabadiliko ya hali ya hewa sio jambo la mzaha hivyo serikali inatakiwa kuwa na sera madhubuti zitakazo wawezesha wananchi kukabiliana na madhara yatokanayo na janga hilo ili kujitahidi kuirejesha ardhi na mazingira yetu kwa ujumla katika hali bora
 Wanafunzi kutoka vyuo vikuu mbalimbali jijini wakitoa maoni yao katika mjadala wa wazi uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee ambapo wamelalamikia baadhi ya Sera za Serikali zisizotekelezeka wakatu wa maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa kusheherekea miaka 67