Watoto 3 wapoteza maisha Dar , TMA yawatoa hofu wakazi kuhusu Tsunami


WATOTO watatu wamefariki dunia kutokana na sababu ya kunyehsa mvua kubwa juzi jijini Dar es Salaam Wawili kati yao ni wa familia moja hao ni Aron Sadogi (7) na mdogo wake Antony wa miezi tisa ambao walikufa baada ya mvua kudondosha nyumba yao eneo la Mtoni Kijichi


Mwingine ni Hadija Ally Shamuhuna (8), mwili wake ulisombwa na maji na mwili huo ulipatikana jana jioni katika maeneo hayo

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, David Misime alithibitisha vifo hivyo na ksuema vifo vyote violitokea juzi jioni vimesababishwa na mvua kubwa iliyonyesha juzi jioni maeneo mengi ya jiji

Mvua kubwa zilinyesha na ksuababisha maeneno mengi kujaa maji na uharibifu wa miundombinu uliotokana na mvua hizo
Kufuatia mvua hizo zilizonyesha juzi ambazo zilileta hofu jijini Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetangaza kutokuwepo kwa tishio la Tsunami nchini na kuwataka wananchi waishio pembezoni mwa bahari kurejea makwao na wale wanaoendesha shughuli za baharini waendelee kama kawaida.

Juzi jioni mamlaka hiyo ilitoa tahadhari ya kutokea tsunami kutokana na matetemeko mawili yaliyotokea katika Jimbo la Aceh nchini Indonesia, hali ya mtafaruku iliibuka jijini Dar es Salaam huku baadhi yao wakikimbia nyumba zao.

Mamlaka hiyo imesema kutokana na muda wa kutokea tsunami kupita bila madhara yoyote na utabiri ukionesha hali kuwa shwari

Juzi Jiji la Dar es Salaam halikuwa shwari na wakazi kuwa na hofu na ksuababisha wafanyakazi wa katikati ya jiji kuondoka mapema kazini kutokana na hofu