Fumanizi
kati ya mwanafunzi wa kike na fataki aliyefahamika kwa jina la Mustafa Kachenga
(pichani) anayedaiwa ni dereva katika Wizara ya Ujenzi lililotokea kwenye
nyumba ya kulala wageni, Manzese jijini Dar, mambo mazito yameibuka, shuka na
mistari ya habari hii.
Kwa mujibu
wa vyanzo vyetu kutoka jeshi la Polisi, dereva huyo anayemwendesha kigogo wa
wizara hiyo ni baba mdogo wa mwanafunzi huyo ambaye jina lake tunalihifadhi.
Vyanzo hivyo
vimedai kuwa, mwanafunzi aliyebambwa na Kachenga anasoma kidato cha pili katika shule moja
iliyopo Kiluvya wilayani Kisarawe mkoani Pwani, anamwita Kachenga ‘dingi’ mdogo.
Habari
zinazidi kudai Kachenga alitoboa ukweli huo baada ya kubanwa wakati alipokuwa
akihojiwa na askari wa Kituo cha Magomeni jijini Dar mara baada ya kutiwa
mbaroni.
“Mwanafunzi
yule ni mtoto wa kaka yake Kachenga ambaye, kaka mtu aliamini mwanaye atakuwa
katika mikono salama kwa baba yake lakini jamaa ameamua kumgeuzia kibao,”
kilidai chanzo kimojawapo.
Ikadaiwa
kuwa, baada ya Kachenga kupewa mtoto huyo alikuwa akiishi naye nyumba moja
Kiluvya huku akimsomesha katika shule moja ya sekondari katika maeneo hayo.
Habari hizo
zimedai kwamba Kachenga ameoa na anaishi na mkewe pamoja na mwanaye huyo lakini
mke wake hakuweza kugundua kilichokuwa kikiendelea hadi pale alipopata taarifa za kubambwa kwa
mumewe na mwanaye huyo .
Awali
hatukujua kama jamaa ameoa, tuligundua baada ya mkewe kufika kituoni na kuangua
kilio kana kwamba kulikuwa na msiba,” kiliendelea kutoboa chanzo chetu kingine.
Taarifa
zinasema kuwa, baba mzazi wa mwanafunzi huyo anaishi katika kijiji kimoja
kilichopo mkoani Tanga na alimtoa mwanaye akiamini kuwa angeweza kusoma vizuri
tofauti na kama angeendelea kuwa kijijini.
Kachenge
alibambwa na polisi saa tano asubuhi baada ya wananchi wanaoishi karibu na gesti
hiyo kutoa taarifa mara walipomuona akizama ndani na denti huyo.
Wananchi hao
walidai kuwa, Kachenga alikuwa akifika hapo mara kwa mara huku akiwa na binti
huyo anayevalia sare za shule na yeye akiendesha gari lenye usajili wa namba za
serikali.
Kachenga
hakuamini macho yake pale alipovamiwa na polisi katika chumba namba tano
alichokuwa amejifungia na mwanafunzi huyo, aliishiwa nguvu na kujaribu kuomba
msamaha, wakati binti yake alizimia kutokana na tukio hilo la aibu.
Dereva huyo
alichukuliwa na wanausalama hadi Kituo cha Polisi Magomeni. Kamanda wa Polisi
Kanda Maalum ya Kinondoni, Charles Kenyela alikiri kuwepo kwa tukio na kwamba
jeshi lake linamshughulikia.