GRAND MALT YAKABIDHI ZAWADI KWA WASHINDI WA SHINDANO LA EXCEL WITH GRAND MALT MKOANI DODOMA JANA JIONI


Meneja wa Kinywaji Cha Grand Malt Madam Consolata Adam akitoa Shukrani kwa Uongozi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma kwa kuweza kukubali kuruhusu wanafunzi wake kushiriki katika shindano la Excel with grand malt Pembeni ni Mshauri wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma Mh Manongi katika Tamasha la Kukabidhi zawadi kwa washindi waliopatikana katika shindano la excel with grand malt


Mshauri wa wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) akitoa shukrani kwa kampuni ya bia ya Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha grand malt ambao waanzilishi wa shindano la excel with grand lililofikia tamati jana jioni mkoani Dodoma ambapo Chuo Cha elimu ya Biashara Tawi la Dodoma (CBE) na UDOM ndio vyuo pekee vilivyoshiriki katika Shindano hilo katika Mkoa wa Dodoma


Mshindi Wa Tuzo ya Excel with grand malt Kutoka Chuo Cha Elimu Ya Biashara tawi la Dodoma Akipokea zawadi ya kitita cha Shilingi laki tano kutoka kwa mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini  mara baada ya kuibuka mshindi katika kipengele cha Mazingira


Washindi wa Tuzo za excel with grand malt kutoka chuo cha elimu ya biashara tawi la Dodoma wakiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa kampuni ya Bia ya Tanzania (TBL) na Meneja wa Kinywaji ch Grand malt Bi Consolata Adam(Wa tatu Kushoto waliosimama) Mara baada ya Kukabidhiwa Zawadi zao jana jioni ambapo shindano hilo limefikia tamati na kuhitimishwa katika viwanja vya michezo vya Chuo Kikuu Cha Dodoma


Mshindi wa Pili Katika Kipengele Cha utamaduni na burudani kutoka Chuo Kikuu Cha Dodoma Bi Nyaki akipokea kitita cha shilingi laki moja na nusu mara baada ya kuibuka mshindi wa pili


Mshindi wa Pili Katika kipengele cha Mazingira Kutoka Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) Stambuli Athuman akiwa amebebwa juu juu na mashabiki wake mara baada ya kutangazwa mshindi


Washindi wa tuzo za excel with Grand Malt kutoka Vyuo vya CBE na UDOM wakiwa katika Picha ya Pamoja na Wafanyakazi wa kampuni ya Bia ya Tanzania(TBL) na Mwakilishi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini



Michezo mbalimbali ilikuwepo pia


Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Prof JAY akitoa burudani kwa mashabiki wake wa UDOM katika tamasha la kikabidhi zawadi kwa washindi wa excel with grand malt lililofanyika katika viwanja vya UDOM

Shukuran za dhati zimwendee JOSEPH LUKAZA