Lengo la kuwakutanisha wasanii hao wazee ni kusisitiza upendo uliodumu kwa muda mrefu kati ya Tanzania Bara na Visiwani ambao hivi karibuni uliingiwa na dosari baada na wanachama wa kundi la Uamsho Zanzibar kuandamana kupinga Muungano.
Watu kadhaa walijeruhiwa na huku baadhi ya mali zikiharibiwa kwa kuchomwa moto.
Hivyo, show hiyo ni ishara ya kuwa wasanii wanauchukulia Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa umuhimu mkubwa.
Kundi la Wakacha litafanya uzinduzi pia wa ngoma yao mpya huku likipewa support na ‘Bibi’ hao usiku wa leo.
Hii ni show kati ya bara na Zanzibar yaani muungano ndo mantiki ya show..so pale pia tuta introduce nyimbo.” Cyrill aka Kimikaze wa Wachacha Ent ameuambia mtandao huu.
Ili kunogesha zaidi usiku huo na kuifanya kuwa show tofauti, wameamua kuwaleta pamoja wasanii hao ambao hata hivyo aina ya nyimbo wazifanyazo ni tofauti.
Kukutana kwao leo hii pengine kutawaweka karibu zaidi na kuzaliwa uwezekano wa wao kufanya wimbo wa pamoja siku za usoni.
Kama wakifanya ngoma ya pamoja bila shaka Bi.Kidude atamwelekeza Bibi Cheka utunzi wa kiutuuzima zaidi na unaoendana na umri wao.
Hii itakuwa mara ya kwanza kwa Bi.Kidude kutumbuiza kwenye klabu ya usiku jijini Dar es Salaam tofauti na mwenzie Bibi Cheka aliye karibu zaidi na vijana wa Said Fella.