KOSCIELNY AJITIA KITANZI ARSENAL.
BEKI wa klabu ya
Arsenal, Laurent Koscielny amekubali kusaini mkataba wa muda mrefu na
klabu hiyo yenye maskani yake kaskazini mwa jiji la London, Uingereza.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa ambaye ana umri wa miaka 26
amejitengenezea nafasi katika kikosi cha kwanza kwenye klabu hiyo
kutokana na kiwango bora ambacho amekuwa akionyesha toka alipojiunga
miaka miwili iliyopita. Uamuzi wa beki huyo umekuja baada ya
mshambuliaji nyota wa kimataifa wa Uholanzi, Robin van Persie kutangza
kuwa hataki kusaini mkataba mwingine. Mkataba wa sasa wa Van Persie
unaisha mwishoni mwa msimu ujao na mchezaji huyo amedai kuwa anataka
changamoto nyingine baada ya miaka nane ya kuitumikia klabu hiyo. Meneja
wa klabu hiyo, Arsenal Wenger amesema kuwa hatma ya mchezaji huyo
iamuliwe kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi inayotarajiwa kuanza
Agosti 18 mwaka huu huku klabu za Manchester United, Manchester City na
Juventus ambazo zote zimekuwa zikimuhitaji.