Askari
Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) watakaoshiriki kwenye gwaride
wakati wa maadhimisho ya siku ya mashujaa wakiendelea na mazoezi katika
viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam.
Mkuu
wa mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki (katikati) akiongea na
waandishi wa habari Katika viwanja vya Mnazi mmoja leo jijini Dar es
Salaam kueleza namna mkoa ulivyojipanga kufanikisha sherehe za
maadhimisho ya siku ya mashujaa itakayofanyika kitaifa tarehe 25, Julai
2012 katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam
Askari
wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakitoa heshima kwenye mnara
wa kumbukumbu ya Mashujaa katika viwanja vya mnazi mmoja leo ikiwa ni
sehemu ya maandalizi ya sherehe za maadhimisho ya kumbukumbu ya
mashujaa.
Kiongozi
wa mabalozi wan chi za Afrika wanaoishi nchini Tanzania Balozi Juma
Mpango kutoka Congo DRC akiweka shada la maua kwenye mnara wa
kumbukumbu ya mashujaa leo jijini Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya
maandalizi ya sherehe ya siku ya mashujaa itakayofanyika tarehe 25,
Julai 2012.Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.
Wananchi
wa mkoa wa Dar es salaam wameombwa kujitokeza kwa wingi wakati wa
sherehe za maadhimisho ya kumbukumbu ya Siku ya Mashujaa itakayofanyika
kitaifa katika viwanja vya Mnazi mmoja tarehe 25 Julai 2012 jijini
Dar es salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam , Mkuu wa mkoa wa Dar
es salaam Saidi Meck Sadiki amesema maandalizi ya maadhimisho hayo
yamekamilika na kufafanua kuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo atakuwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete.
Amesema
katika maadhimisho hayo kwa upande wa mkoa wa Dar es salaam baadhi
ya barabara zitafungwa ikiwemo barabara ya Nyerere, Uhuru na Bibi Titi
Mohamed ili kuhakikisha usalama kwa wale wote watakaohudhuria
maadhimisho hayo na kuongeza kuwa katika kuboresha maadhimisho hayo
kamati ya maadhimisho itaweka luninga katika maeneo yote muhimu ili
kuwawezesha wananchi kuona yanayotendeka wakati wa maadhimisho hayo.
Aidha
Bw. Meck Sadiki amesema kuwa maadhimisho hayo ni kumbukumbu muhimu
katika historia ya Tanzania kwa kuwaenzi mashujaa waliojitoa muhanga
katika jitihada za kuikomboa na kuilinda Tanzania.