Msanii wa filamu bongo Geofrey Kusila baada ya kufanyiwa sherehe ya kushtukiza na kimwana Salma Jabu ‘Nisha’, na baadaye ikidaiwa kuwa wao ni wapenzi, ingawa kwa upande wa Kusila anakunusha taarifa hizo.Kauli ya kukanusha kwa Kusila, imekuja baada ya kuongea na mtandao huu, ambapo alidai kuwa yeye ni mume wa mtu na hana mahusiano yoyote na Nisha.
Msanii huyo alidai kuwa mara nyingi wanakutana kwenye filamu na sasa wapo mbioni kuachia kazi mpya waliyofanya pamoja inakwenda kwa jina la ‘Mchana wa Kiza’.
Wakati huo huo mwandishi alimtafuta Nisha ili kueleza kwa upande wake, ambapo alidai kuwa ingawa jamaa anakataa lakini ukweli unajulikana kwamba wao ni wapenzi.
“Mapenzi yapo ndiyo tumecheza kwenye filamu, lakini hata nje yapo hivyo sijui kitu ambacho watu wanazungumzia pia nashangaa kwanini Kusila anakataa kusema ukweli,” alidai.