Afisa
Muandamizi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii Tanzania, Juma Kimtu
akimkabidhi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi
Mchango wa Maafa wa Sh10m ofisini kwake Mbweni, Zanzibar. Nyuma yake ni
Meneja Msuluhishi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar {ZSSF}, Khamis
Phil Phil Than.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi, Seif Ali Iddi akipokea mchango wa
Maafa wa Sh10m kutoka kwa Meneja Msuluhishi wa Mfuko wa Hifadhi ya
Jamii Zanzibar { ZSSF } Khamis Phil Phil Than katika Ofisi yake iliyopo
Baraza la Wawakilishi Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewanasihi
Wananchi kuendelea kuiamini Serikali katika kupokea Taarifa zake hasa
wakati wa kutokea Majanga na Maafa.
Nasaha hizo amezito hapo katika Ofisini yake iliyopo Baraza la
Wawakilishi Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar wakati akipokewa mkono
wa Pole kutoka kwa Taasisi mbali mbali za Umma na Kijamii.
Salamu hizo za mkono wa pole zimetolewa kwa Balozi Seif na Uongozi wa
Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar { ZSSF } na ule wa Hifadhi ya Taifa
ya Jamii ya Tanzania { NSSF } ambapo kila moja ilikabidhi mchango wa
Shilingi Milioni kumi { 1,000,000/- }.
Balozi Seif alisema Jamii kujenga tabia ya kuiamini Serikali
hupelekea kuwepuka kuchanganywa wakati wa kupokea Taarifa hizo kutoka
vyombo vya Habari vinavyopokea Baadhi ya Taarifa zisizo rasmi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliupongeza Uongozi wa mifuko hiyo
ya Hifadhi ya Jamii Bara na Zanzibar kwa kufikiria jambo hilo muhimu la
kutoa mchango ambalo Taifa linahitaji kuungwa mkono katika kukabiliana
nalo.
Aliuhakikishia Uongozi wa Taasisi hizo kwamba michango hiyo
itasimamiwa vyema kwa ajili ya kuwafika waliohusika kwa kutumia
utaratibu uliotumika wakati wa ajali iliyotokea Mwaka jana.
Alisema licha ya zoezi la uokozi kuwa na gharama kubwa lakini Serikali
inaendelea kutoa huduma zote za mazishi na usafirishaji wa maiti
zinazopelekwa Tanzania Bara ambazo zilipatikana kutokana na ajali ya
Meli ya M.V Skagit hapo juzi.
Aliongeza kuwa shughuli hiyo ikiwemo gharama za vyombo, mafuta, Chakula
na uokozi zinahitaji kuungwa mkono na taasisi na jumuiya ya kiraia
ndani na nje ya Nchi. “ Serikali imeshachukua jukumu la kuzizika zile
Maiti zilizoshindwa kutambulika hadi sasa, kuzisafirisha maiti tatu
hadi Tanzania Bara pamoja na familia nne wakati maiti moja ya raia wa
kigeni bado haijatambulika”. Alifafanua Balozi Seif.
Alisisitiza kwamba katika juhudi za kukabiliana na tatizo hilo
wazamiaji wa Israel walioko Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja wameamua
kusaidia kazi ya uokozi kwenya Meli hiyo ili kuendelea kutafuta miili
ya Watu iliyopotea.
Mapema
Meneja Msuluhishi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar { ZSSF } Ndugu
Khamis Phil Phil Than alisema yapo mambo mengi kwenye tukio hilo la
Maafa ambayo yanahitajika kupata msukumo kutoka kwa Washirika, Taasisi
na Jumuiya za Kiraia. Ndugu Phil Phil alisema mfuko wa Hifadhi ya Jamii
Zanzibar umekuwa mstari wa mbele katika kutekeleza majukumu yake
yaliyolenga zaidi kwenye eneo la Jamii.
Naye
kwa upande wake Ofisa Muandamizi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii
Tanzania { NSSF } kutoka Makao Makuu Mjini Dar es salaam Nd. Juma
Kimtu alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba Taasisi hiyo
imeamua kutoa mchango huo baada ya kuona uzito Maafa yaliyotokea
ambayo yameigusa Jamii yote.
Ndugu
Kimtu alisema Serikali kwa kuwa ni ya watu haina budi wakati wote
kusaidiwa hasa katika masuala ya Majanga na Maafa ambayo kwa kiasi
kikubwa huigusa Jamii yote.
Na
Othman Hamisi Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili Wa Rais Zanzibar