Lucas Moura.
MATUMAINI ya meneja wa
klabu ya Manchester United kumsajili Lucas Moura kwa paundi milioni 30
yamefutika baada ya klabu hiyo kuonywa kuwa kiungo huyo wa kimataifa wa
Brazil hawezi kuondoka katika klabu yake ya Sao Paulo. Akiwa tayari
amewasajili Shinji Kagawa na Nick Powell katika kipindi hiki cha majira
ya kiangazi, Ferguson alikuwa na matumaini ya kumsajili kiungo huyo
mwenye umri wa miaka 19 kwa hela nyingi. Lakini Ferguson amechanganywa
na suala la uhamisho wa Moura ambaye kwasasa yuko jijini London na
kikosi cha Brazil kwa ajili michuano ya Olimpiki baada ya kukataliwa kwa
mara ya pili sasa. Wakala wa Moura, Wagner Ribeiro sasa amepigilia
msumari wa mwisho katika jeneza la United baada ya kusisitiza kinda huyo
anahitajia kiasi cha fedha ambacho timu hiyo haiwezi kufikia hivyo
atabakia katika klabu yake ya Sao Paulo.