Habari
za Uhakika zimeifikia blog hii kuwa Rais John Atta Mills wa
Ghana, amefariki dunia jana jumanne 24 julai 2012 mjini Accra,Ghana.
Umati wa maelfu ya watu mapema jana walikua wamezunguka katika hospital ya jeshi ya 37 Military Hospital iliyopo mjini Accra.
Marehem
Rais John Atta Mills (68) alifariki jana mapema baada ya kupelekwa
katika hospital hiyo ya kijeshi,mpaka sasa haijulikani ugonjwa gani
ulikua unamsumbua.
Taifa
hilo la Ghana linakumbwa na msiba huu wakati wakielekea katika
uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika mwezi Desimba mwaka huu.
Mungu amlaze pema peponi Rais John Atta Mills(RIP).